Friday, 29 December 2017

ASIYE SIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU.

Tags
Anaandika Mch. Francis Mbalase wa Kanisa la Pentekoste -
Mbeya
Chonde chonde CCM,mmekosea kujibu maneno ya Askofu kwa matusi na kejeli. Kama mnajua kuombewa, pia mjue na kutubu. Kutubu sio dhambi ni kupatana na aliyekupa uhai.
Tunaofahamu mambo ya rohoni CCM mmekurupuka kumjibu Baba Askofu, mngejitathimini kwanza.Wala ktk hilo la Askofu, kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kujibu. Maana kukaa kimya nayo ni hekima.
Majibu mliojibu yote hayana mashiko na hayakujibu hoja za Askofu Kakobe (aibu tu)
Wapo viongozi wa dini wengi tu waliikemea serikali, waliopuuza waliiingiza jamii ktk utumwa wa kutawaliwa na taifa lingine.
Wakitubu Mungu aliwasamehe na kuwainulia kiongozi aliyewaokoa. Inamaana walipoingia utumwani, viongozi wale wakaidi walipoteza haki ya kutawala au kuuwawa.
Maaskofu wetu kuwaeleza kuwa mtubu wanawapenda sana, nia yao ni njema ili msiangamie. Badala yake mnawatusi,.. kweli?Mnawahoji kama wahalifu badala ya kuwaomba ushauri. Kiimani mnajipalia makaa ya moto. TUBUNI TU.
Musa alimkemea Farao mfalme wa Misri (Kut 10: 1-29), Elia Mtishbi alimkemea Ahabu (1Fal 17:1-24; 18:1-46) , Shadrack na wenzie (Dan 3:3-30) , Yohana mbatizaji kwa Herodi (Mt 14:1-12),Yesu mwenyewe alikemea mfalme kwa kumwita mbweha nk. (LK 13:31,32); Yohana Mbatizaji alionya askari na watumishi wengine wa Umma (mfano wa TRA leo yaani watoza ushuru) - LK 3:7-14.
Kiongozi yoyote wa kiroho ni wakili wa Mungu (kwa niaba ya Mungu). Ukisoma Tito 3:1 neno la Mungu linasema:
......UWAKUMBUSHE WATU KUNYEKEA KWA WENYE UWEZO NA MAMLAKA,NA KUTII,NA KUWA TAYARI KWA KILA KAZI NJEMA, na
WARUMI 13:1. Muagizaji wa haya au msimamizi ni mchungaji. Hivyo mambo yasipoenda sawa ni wajibu ayakemee maana yeye ni mamlaka ya mbinguni.
Tuondoe chuki na ukabila na udini ile Taifa letu Mungu aliinue. Naomba sasa watu wa madhehebu yote liombee sana Kanisa na Taifa na acheni kuombea watawala wasio na toba
1 Samweli 16:1 BWANA AKAMWAMBIA SAMWELI,HATA LINI UTAMLILIA SAULI,IKIWA MIMI NIMEMKATAA ASIWAMILIKI ISRAEL? Watu wasiokuwa na toba ni kuwaacha, maana hawawezi kwenda na BWANA.
MAASKOFU WOTE WAMESIMAMIA UTAIFA.Fahamu muda wote walikaa kimya,wameona uharibufu kuwa unakuja, tiini.
Ccm wamemkejeli Kakobe eti aache dini aje kwenye siasa. Naomba mfahamu kuwa siasa na dini vinakwenda pamoja na mtu wa dini hakwepi siasa. Najua hilo mnalijua sana na ndio sababu mkamteua Mchungaji Getrude Rwakatale kuwa mbunge. Mkisema mtumishi hahusiki na siasa,mnajionyesha mlivyo na unafiki. Bado hata wapinzani yupo Mch Msigwa. Kwa Askofu Kakobe imekuwa nongwa? Tena ameongelea mhimili wa taifa.
Mwisho niwaombe viongozi wangu, MTUBU TU.

Wednesday, 27 December 2017

Tags
http://sw.radiovaticana.va/news/2017/12/27/askofu_isaac_a_massawe_ateuliwa_kuwa_askofu_mkuu_jimbo_kuu_la_arusha/1356489

Tuesday, 26 December 2017

ASKOFU KAKOBE AIJARIBU SERIKALI.

Tags
   Askofu Kakobe Amewataka Viongozi wa Serikali Kuongoza kwa kufuata katiba ya Nchi.

Askofu Kakobe Akiwa anatoa Mahubiri yake Wakati wa Ibada ya Noeli,Amesema Viongozi wa Serikali Wanaongoza Nchi kwa kuto fuata Matakwa ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kwa kuzuia Vyama Vya Siasa kufanya kazi zake wakati vyama hivyo Vipo kikatiba.

  Askofu Kakobe Amesema Kutokana na Uvunjaji huo wa katiba ya nchi Kunaweza kuleta Mafarakano Ktk Nchi Kwani Amani iliyopo ni Matunda ya Waasisi wa Taifa hili Kuheshimu Katiba  na Sheria zilizozopo.

Pamoja na Hilo Askofu huyo ameishauri Serikali kama inaona Mfumo wa Vyama vingi haufai Bora kupeleka mswada Bungeni ili Itungwe Sheria ya kufuta Mfumo wa Vyama vingi ambao kwa sasa Katiba inautambua,Kwani Kuvizuia vyama hivyo kufanya kazi yake ni Kutenda Dhambi kwani hata Mungu pia Anaheshimu Sheria.

 Askofu Kakobe pia Amewashauri Viongozi kukubali kukosolewa kwani hata Mungu anasemwa vibaya Lakini Hawaadhibu Wanao Msema vibaya.

KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;

USIPANGE KUIKOSA