Askofu Kakobe Amewataka Viongozi wa Serikali Kuongoza kwa kufuata katiba ya Nchi.
Askofu Kakobe Akiwa anatoa Mahubiri yake Wakati wa Ibada ya Noeli,Amesema Viongozi wa Serikali Wanaongoza Nchi kwa kuto fuata Matakwa ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kwa kuzuia Vyama Vya Siasa kufanya kazi zake wakati vyama hivyo Vipo kikatiba.
Askofu Kakobe Amesema Kutokana na Uvunjaji huo wa katiba ya nchi Kunaweza kuleta Mafarakano Ktk Nchi Kwani Amani iliyopo ni Matunda ya Waasisi wa Taifa hili Kuheshimu Katiba na Sheria zilizozopo.
Pamoja na Hilo Askofu huyo ameishauri Serikali kama inaona Mfumo wa Vyama vingi haufai Bora kupeleka mswada Bungeni ili Itungwe Sheria ya kufuta Mfumo wa Vyama vingi ambao kwa sasa Katiba inautambua,Kwani Kuvizuia vyama hivyo kufanya kazi yake ni Kutenda Dhambi kwani hata Mungu pia Anaheshimu Sheria.
Askofu Kakobe pia Amewashauri Viongozi kukubali kukosolewa kwani hata Mungu anasemwa vibaya Lakini Hawaadhibu Wanao Msema vibaya.
Tuesday, 26 December 2017
ASKOFU KAKOBE AIJARIBU SERIKALI.
Diterbitkan December 26, 2017
Tags
Artikel Terkait
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;
USIPANGE KUIKOSA
EmoticonEmoticon