Friday, 6 April 2018

MBUNGE AHOJI MAMBO MAZITO.

Tags

Monday, 2 April 2018

BURIANI WINNIE MANDELA.

Tags
PUMZIKA KWA AMANI WINNIE MANDELA: MWANAMKE JASIRI NA MPAMBANAJI BARANI AFRIKA.

Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81.

Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.

Alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe - Nelson Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw. Mandela.

Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27.

Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata.

Msemaji wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa: "Amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa mara tangu mwanzoni mwa mwaka.

"Alifariki kwa amani mapema Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake."

Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama "ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi," kwa mujibu wa AFP.

Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipatia umaarufu mkubwa katika siasa nchini Afrika Kusini.

Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa.

Katika kipindi chote cha miaka 27 mumewe alipokuwa gerezani bila matumaini ya kuachiwa huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa mwaka 1964, Bi Winnie alilazimika kubeba jukumu la ulezi wa watoto na pia kuendeleza kampeni za kisiasa kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao waachiwe huru hasa mumewe.

"Kamwe hatutapoteza matumaini na watu wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila shaka tunatarajia kwamba kazi itaendelea," alisema wakati huo.

Kutokana na hayo Bi Winnie Mandela alilazimishwa kusalia tu huko Brandford katika jimbo lao la Orange Free katika miaka ya 70 baada ya operesheni mojawapo za kupambana na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi kama the Soweto Uprising.

Kama ilivyomtokea mumewe, Bi Winnie alifungwa gerezani, na hata kuwekwa katika kizuizi cha pekee yake ambacho ni mojawapo ya vifungo vigumu zaidi gerezani vinavyowaathiri wafungwa kisaikolojia.

Lakini baada ya kuachiwa kwake mtindo wa mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi ulianza kupata sifa mbaya hasa pale alipoonekana kuendekeza tabia ya kuwavisha tairi shingoni wale waliolengwa kwa tuhuma za usaliti na kisha kuwachoma moto.

"Kwa 'mikufu yetu' tutaikomboa nchi hii," alizoea kusema.
Mambo yalizidi kumwendea mrama kutokana na matendo ya baadhi ya walinzi wake katika kile kikundi kilichojulikana kama the Mandela United Football Club.

Walipatikana kuhusika katika kitendo cha kumteka nyara na kumuua kijana mmoja mwenye umri wa miaka 14 aitwae Stompie Moeketsi -kwa tuhuma za kwamba alikuwa akitoa siri kwa maadui zao.

Japo Bi Winnie Mandela aliepuka hukumu ya kifungo jela - baadaye tume ya ukweli na maridhiano iliyoongozwa na askofu Desmond Tutu, iliyokuwa inachunguza ukweli kuhusu matendo tata katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta maridhiano, ilimpata Bi Mandela na hatia ya kutowajibika kisiasa wala kimaadili wakati wa kitendo hicho.

Licha ya misukosuko hiyo Bi Mandela alibaki kuwa mtu muhimu sana katika siasa za Afrika kusini na kuwa mwakilishi muhimu wa wanawake waliopambana kufa na kupona dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi uliokuwa unaendelezwa na Wazungu walio wachache nchini humo.

Katika siku za baada ya uhuru wa Afrika Kusini anakumbukwa zaidi kwa kuwa miongoni mwa wachache katika uongozi wa ANC waliomuunga mkono aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki katika kushutumu na kulaani vikali vitendo vya kuwashambulia wahamiaji wa Kiafrika huko nchini Afrika Kusini.
KUSINI - mashambulio yalibandikwa jina xenophobic attack.

Pia amekuwa muungaji mkono mkubwa wa kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema, kilichojimegua kutoka ANC ambacho kilimkosoa vikali Rais aliyelazimika kung'atuka madarakani Bw. Jacob Zuma.

Historia ya Bi Winnie Madikizela Mandela, hadi kifo chake inabaki kukumbukwa zaidi kama Mama wa taifa la Afrika Kusini aliyesimama kidete dhidi ya ubaguzi wa rangi katika umri wake wote.

APUMZISHWE KATIKA AMANI YA BWANA.




Sunday, 1 April 2018

ASKOFU MKUDE AWALILIA WANAOPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA.

Tags

*************************
Askofu wa jimbo katoliki Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude ametahadhalisha uwepo wa hofu Kubwa kutokana na ukimya usio na maelezo juu ya raia wa Tanzania wanaopotea.

Akizungumza katika homilia yake takatifu Mara baada ya kusomwa barua yake ya kichungaji katika misa ya mkesha wa pasaka usiku wa tarehe 31 kuamkia tarehe 1,Askofu Mkude amesema ukimya usio na maelezo unaoendelea juu ya raia wanaopote a unatia mashaka na unajenga hofu Kubwa

Askofu Mkude amesema raia wanaopotea ni raia walio na familia,Ndugu jamaa na marafiki hivyo kupotea kwao kunapotokea na serikali kukaa kimya bila maelezo yoyote kunajenga hofu.

"Ipo huzuni kubwa kumpoteza Jamaa yake,na ni heri baadae ujue kama amefariki ili umuombee,kuliko kutokujua kabisa mahali alipo,inatia hofu" alisema

"Yesu alipotoweka,(kufa)na siku ya tatu alipoonekana tena(kufufuka)wanafunzi wake walifurahi mno,hivyo tunaitumaini furaha hiyo endapo siku moja Ndugu hawa wataonekana"

Vilevile Askofu Mkude aligusia upotoshaji wa habari za mitandao huku akiita ni kama"kilema Mamboleo".

Akisisitiza juu ya upotoshaji wa mitandao,Askofu Mkude alikumbushia kuhusu uzushi ulioibuka miezi mingi iliyopita juu ya kifo chake wakati akiwa katika matibabu nchini India.

"Nyinyi mtakuwa mashahidi wakati nazushiwa kifo,mlihuzunika sana,hata Arusha nasikia walishanisomea Misa,lakini mliponiona tena mlifurahi....japo nilikuwa natembelea fimbo,sasa hata fimbo sina tena,mmefurahi" alisema Askofu Mkude

"Furaha hiyo ndiyo tunayotarajia wataipata Ndugu wa raia waliopotea" alikazia

Lakini Askofu Mkude alisema ameomba barua yake hiyo isomwe Tanzania nzima ili ujumbe huo wa kupotea kwa raia uwafikie watu wote.

Mwisho Askofu Mkude alitaja vile alivyoviita vilema mamboleo ikiwemo suala la "siasa bila kanuni na sheria"

ASKOFU NGALALEKUMTWA AWAOMBA WAUMINI MAMBO MATATU.

Tags
Askofu Wa Jimbo Katoliki La Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa Akihitimisha Misa ya Sherehe Ya Pasaka,katika Kanisa La Kiaskofu Kihesa Iringa;Amewaomba Waumini Mambo Matatu.
 
    Askofu Ngalalekumtwa Amewaomba Waumini Kuombea Familia na Jumuiya zao Ziwe Na Hali Njema ya kiuchumi,Ili kuondokana na Ugumu wa Maisha unao zikabili Familia hizo.
Pia Ameomba Jambo la Pili Kuombea Amani na Kuiombea Serikali ya Rais Magufuli ili iwe ni Serikali yenye Huruma Kwa Raia inaowaongoza,Askofu Ngalalekumtwa Amesema Uongozi ni Kazi ngumu Hivi amewataka Waumini Kuiombea Serikali ili Iongoze kwa Kufuata Misingi ya Haki.

  Jambo la Tatu Amewaomba Waumini Hao Kuombea Hali Njema ya Hewa.Amesema Mvua zilizo Chelewa kunyesha zikikata Mapema,Mazao Yanaweza kuharibika.


KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;

USIPANGE KUIKOSA