*************************
Askofu wa jimbo katoliki Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude ametahadhalisha uwepo wa hofu Kubwa kutokana na ukimya usio na maelezo juu ya raia wa Tanzania wanaopotea.
Akizungumza katika homilia yake takatifu Mara baada ya kusomwa barua yake ya kichungaji katika misa ya mkesha wa pasaka usiku wa tarehe 31 kuamkia tarehe 1,Askofu Mkude amesema ukimya usio na maelezo unaoendelea juu ya raia wanaopote a unatia mashaka na unajenga hofu Kubwa
Askofu Mkude amesema raia wanaopotea ni raia walio na familia,Ndugu jamaa na marafiki hivyo kupotea kwao kunapotokea na serikali kukaa kimya bila maelezo yoyote kunajenga hofu.
"Ipo huzuni kubwa kumpoteza Jamaa yake,na ni heri baadae ujue kama amefariki ili umuombee,kuliko kutokujua kabisa mahali alipo,inatia hofu" alisema
"Yesu alipotoweka,(kufa)na siku ya tatu alipoonekana tena(kufufuka)wanafunzi wake walifurahi mno,hivyo tunaitumaini furaha hiyo endapo siku moja Ndugu hawa wataonekana"
Vilevile Askofu Mkude aligusia upotoshaji wa habari za mitandao huku akiita ni kama"kilema Mamboleo".
Akisisitiza juu ya upotoshaji wa mitandao,Askofu Mkude alikumbushia kuhusu uzushi ulioibuka miezi mingi iliyopita juu ya kifo chake wakati akiwa katika matibabu nchini India.
"Nyinyi mtakuwa mashahidi wakati nazushiwa kifo,mlihuzunika sana,hata Arusha nasikia walishanisomea Misa,lakini mliponiona tena mlifurahi....japo nilikuwa natembelea fimbo,sasa hata fimbo sina tena,mmefurahi" alisema Askofu Mkude
"Furaha hiyo ndiyo tunayotarajia wataipata Ndugu wa raia waliopotea" alikazia
Lakini Askofu Mkude alisema ameomba barua yake hiyo isomwe Tanzania nzima ili ujumbe huo wa kupotea kwa raia uwafikie watu wote.
Mwisho Askofu Mkude alitaja vile alivyoviita vilema mamboleo ikiwemo suala la "siasa bila kanuni na sheria"
Sunday, 1 April 2018
ASKOFU MKUDE AWALILIA WANAOPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA.
Diterbitkan April 01, 2018
Tags
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;
USIPANGE KUIKOSA
EmoticonEmoticon