Saturday, 30 September 2017

UTALII NI NGUZO YA UCHUMI WA VIWANDA.

Tags
Wapendwa Wananchi Wote Mnakaribishwa katika Maonyesho
Ya Utalii Yanayo endelea Katika
Viwanja Vya Kichangani vilivyopo
Kihesa Mkoani Iringa.

Kwa namna ya Pekee Tunawakaribisha
Katika Banda la VETA Mkoa wa Iringa,ili Mjionee Namna VETA inavyoweza Kuzalisha Mafundi wa Fani Mbali mbali.
   (1)Baadhi ya Bidhaa zilizotengenezwa         na Chuo cha VETA Iringa.
   (2) Mkuu wa Chuo Cha VETA                      Iringa,Eng Raphael Ngwandu                    akimtembeza Mgeni Rasmi                        Mheshimiwa Waziri Maghembe              alipotembelea banda la VETA.
      (3) Mwanachuo wa VETA                                 Iringa,Anatalia Luhala Akiwa                   na Batiki zilizo tengenezwa
             VETA.

  (4)Mkuu wa banda la VETA Mhandisi          G.Mmole akitoa                                             Maelekezo kwa mmoja wa walio             tembelea banda la VETA.
  (5)Wanachuo Fani ya Mapishi                        Wakiandaa Chakula kama sehemu
        Ya mazoezi kwao.

Thursday, 28 September 2017

MHASHAMU BABA ASKOFU SEVERIN NIWEMUGIZI ATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA ILIYOPENDEKEZWA NA TUME YA WARIOBA UENDELEE.

Tags


Askofu wa Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi.

Askofu Niwemugiza amesema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili, haki na ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.

Akifungua mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya leo Jumatano, Askofu Niwemugizi amesema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri.

Amesema hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye machafuko kwani wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.

Askofu Niwemugizi amesema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.



"Hizi sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni Katiba."

Amesema anatambua jitihada anazofanya Rais John Magufuli katika kupambana na ufisadi na kutaka rasilimali ziwanufaishe wanyonge lakini ni muhimu juhudi hizo zilindwe na Katiba nzuri.

"Rais anafanya mengi mazuri na alipoanza kila mmoja aliona dalili za matumaini lakini juhudi hizo zinaweza zisiwe endelevu kama hakuna ulinzi wa Katiba,”

"Tunahitaji Katiba tena Katiba nzuri ambayo haitaruhusu kuchezewa na yeyote kwa maslahi au matakwa yake binafsi."

Amesema, "Namshauri Rais achunguze kwa makini yatakayozungumzwa kwenye mkutano huu,  ayaone kuwa yana nia njema na ayafanyie kazi.

Tuesday, 26 September 2017

JE!UNAFAHAMU KUHUSU HII?

Tags
Inasemekana vita iliyopiganwa kwa muda mfupi zaidi hapa Duniani,ni kati ya Zanzibar na England. Iliisha ndani ya dakika 38 tangu kuanza kwake,vikosi Vya Askari wa Zanzibar viliamua kukubali kushindwa.Vita hii ilipiganwa mwaka 1896.

JE!UNAFAHAMU KUHUSU HII?

Tags
Inasemekana vita iliyopiganwa kwa muda mfupi zaidi hapa Duniani,ni kati ya Banzi na England. Iliisha ndani ya dakika 38 yangu

JE!UNAFAHAMU KUHUSU HII?

Tags
Inasemekana vita iliyopiganwa kwa muda mfupi zaidi hapa Duniani,ni kati ya Banzi na England. Iliisha ndani ya dakika 38 yangu

Friday, 22 September 2017

MBOWE AONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HALI YA MHE.TUNDU LISSU.

Tags
HOTUBA YA MH MBOWE NA WANAHABARI

"Nianze na habari njema; Tundu Lissu anawasalimu sana. Nimeachana naye Nairobi jana mchana nikamwambia nitazungumza na Watanzania." Mbowe.

''TunduLissu hajawahi kukata kauli toka Siku ya kwanza ya shambulio na hata hali yake ya uelewa iko palepale'' Mbowe

''Mheshimiwa Lissu yupo chini ya ulinzi mkali sana, na hili limefanyika kutokana na watu waliokuwa wakitaka kumdhuru mh Lissu'' Mbowe

''Usalama wa Tundu Lissu ni mkubwa sana ndani na nje ya hospitali ya Nairobi masaa 24'' Mbowe

"Kumekuwa na kauli nyingi sana, ndugu zangu Watanzania pamoja na kiu ya kupata habari hili sio jambo la kuuzia magazeti'' Mbowe.

"Mashine yetu 'Lissu' itarudi barabarani salama kabisa ikiwa timamu, nataka niwaeleze ufahamu wake uko vizuri 100%" Mbowe

"Niwaombe rasmi kwa niaba ya Chama, madaktari, familia kuwaomba sana Watanzania, kauli zisizo rasmi zisipewe nafasi." Mbowe.

"Nisistize kwamba taarifa rasmi za chama zitatolewa na mimi mwenyewe nikiwa ama Dar es Salaam au Nairobi." Mbowe.

"Madaktari wanasema ni miujiza kutoka salama bila kukatwakatwa kwa risasi ktk shambulio kama la Lissu" Mbowe

"Lissu anatibiwa na kundi kubwa la madaktari na ningependa niwatambue waingie kwenye rekodi kwa kazi ya ziada kuokoa maisha ya Lissu." Mbowe

"Kazi kubwa iliyofanywa na madaktari wa dodoma tusiipuuze, ilituwezesha kufika Nairobi akiwa hai. Ilikuwa ni miujiza kila mmoja alishangaa." Mbowe

MBOWE;-kwenye kikao tulichokaa dodoma mimi pamoja na waziri wa afya Ummy Mwalimu,waziri wa mambo ya ndani,katibu wa bunge,naibu spika na spika wa bunge.

MBOWE.-Serikali iliweka msimamo kuwa kama lissu atapelekwa nairobi badala ya muhimbili haitakuwa tayari kugharamia matibabu ya lissu.

MBOWE;-Spika alitamka wazi kuwa bunge haliko tayari kugharamia matibabu ya lissu kama atapelekwa nairobi na spika alisema anajitoa na ananawa mikono.

MBOWE;-huyu ummy mwalimu aliyesema jana kuwa serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya lissu ndiye aliyeweka msimamo kuwa kama lissu atapelekwa nairobi basi serikali haiko tayari kugharamia matibabu yake.

MBOWE;-ummy mwalimu anasema wanaochangisha pesa za matibabu ya lissu ni matapeli mwambieni sisi hatuko kama wao waliokula pesa za rambirambi za kagera tutawatolea hesabu ya pesa zote za michango.

MBOWE-;mpaka sasa pesa ambazo wabunge walitoa nusu ya posho zao spika wa bunge amezitia mfukoni pamoja na kwamba aliomba acaunt ya hospital aziingize lakini mpaka leo spika hajaingiza hizo pesa ambazo wabunge walitoa kwa ajili ya matibabu ya lissu.

MBOWE;-Jaji mkuu suala ya uchunguzi si la mahakama ni la polisi wewe usubiri mahakamani tunakuheshimu sana ,tunapoomba uchunguzi kutoka nje ya nchi inamaana hatuna imani na vyombo vya ndani ..Kwa hiyo si vema sana jaji kutuingilia kwa hili..tunakuheshimu sana nisingependa kumvunjia heshima jaji huyu.

MBOWE-;spika alinipigia simu juzi kuwa wapo tayari kuhudumia kwa masharti matatu..Sharti la kwanza ni mbowe uandike barua ya maombi,,Sharti ya pili ni lissu lazima apelekwa india,,-Sharti la 3 familia iandike barua ya maombi.

MBOWE -;mbunge kutibiwa stahiki yake..mbunge hapaswi kuandika barua ya maombi kutibiwa kwake labda kama anaumwa mke wake au mtoto.

MBOWE-;mpaka sasa gharama za lissu kutibiwa ni zaidi ya milion 122,michango ya lissu ni dolla elfu 22 kutoka kwa watanzania wanaokaa nje,watanzania wa ndani wamechangia  milion 54 za acaunt ya CRDB kwa njia simu ni milion 24.

MBOWE;-kuhusu ulinzi wa lissu msiwe na shida lissu analindwa 24 hours.

MBOWE-;Sisi kama binadamu tuna hisia kutokana na unyama tunaofanyiwa na serikali iliyopo madarakani ,Tuna hisi kuwa waliomshambulia lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama.

Monday, 18 September 2017

WATANZANIA YATUPASA KUOMBA TOBA ILI KUEPUKA LAANA YA MUNGU.

Tags
   Mambo yanayo endelea sasa Hapa nchini,Bila Kufanya Toba naiona ghadhabu ya Mungu juu yetu.Mambo
Ni ya aibu Sababu hata Wanyama
Wanatushangaa.
 
 

Saturday, 9 September 2017

PADRE BAPTIST MAPUNDA (TUNDA LA KANISA)ATOA USHAURI MZITO KWA VIONGOZI WA SERIKALI.

Tags


Padre Baptist Mapunda wa Kanisa Katoliki nchini, amtaka Rais John Magufuli kutambua kuwa bila majadiliano na viongozi wengine wa vyama vya siasa vya upinzani, hatma ya nchi itakuwa mbaya sana siku zijazo. Akitoa mahubiri yake katika Kanisa Katoliki la Manzese, jimbo kuu la Dar es Salaam jana, Padre Mapunda alisema Rais Magufuli awe na busara na kufuata mwenendo wa Nabii Suleimani ambaye katika uongozi wake alikuwa akiomba muongozo wa Mungu na hukujifanya Mungu mtu.

Kwa mujibu wa Padre Mapunda utekelezaji wa majukumu ya kiuongozi yanahitaji kusikilizana baina ya pande zinazokinzana pindi kunapokuwa na sintofahamu kama ilivyo sasa katika taifa.

“Hata Mungu aliwahi kukosolewa na Nabii Musa pale alipotaka kuwaondowa Waisraeli sembuse binadamu tunaoendelea kuishi au viongozi wetu? Hali hiyo inaonesha matakwa ya Katiba mpya yanahitajika kwa haraka sana”, Alisema Padre Mapunda.

Padre Mapunda aliwakumbusha viongozi wa dini wanaotarajia kukutana na rais Magufuli kumsaidia na kumuelekeza namna ya kuongoza nchi.
Alisisitiza kuwa Rais Magufuli na watendaji wake, wanapaswa kuiga mienendo ya Nabii Suleimani ambaye aliomba hekima na msaada kutoka kwa kwa Mungu katika kuongoza watu wake kwa HAKI na kutetea wanyonge.

"Watanzania wasome Biblia na kutambua mafundisho ya Yesu Kristo kwani alikuwa akifanya siasa ambazo zilitetea wanyonge lakini wanasiasa wetu wanapotosha umma, hivyo kanisa lazima likemee mwenendo ambao baadae utaichafua nchi ambayo ni kiota cha amani", Alisema Padre Mapunda.

Alisema, "Siasa bila dini ni sawa na wendawazimu na kusisitiza Nabii Suleimani anapaswa kuigwa na viongozi wa Tanzania kwa sababu katika utawala wake hakujifanya Mungu mtu".


WATANZANIA TUUNGANE KULISAIDIA JESHI LETU LA POLISI,KUWAFICHUA WATU WASIO JULIKANA.

Tags
  Nchi ya Tanzania iliyo sifika kwa
muda mrefu,kama kisiwa cha
Amani imeingiliwa na Mdudu
mbaya sana Ajulikanaye kama
WATU WASIOJULIKANA.

  Watu hawa wasio julikana
wamekuwa,Ni tatizo kubwa sana,
kwani wanasababisha Wananchi
Wakose Amani katika nchi yao.

  Ni muda mrefu sasa zimejengeka Tabia za kihuni ambazo tusipo
 zikemea zitaliingiza Taifa katika
Matatizo Makubwa sana.Tunala-
Zimika kwa umoja wetu kukemea
Hali hii,bila kujali ni watu gani
Wanaofanya mambo haya,Tuna-
takiwa kukemea bila kumwonea
Mtu.Kwa kufanya hivyo tutakuwa
Tumeliokoa Taifa letu.

  Wote mtakuwa Mashahidi kuwa
Kila Leo watendaji wa matukio haya
Wanazidi kuimarisha hizo mbinu zao
Ovu.walianza na kumwagia watu tindikali wakaona haitoshi wakaanza
Kuwateka watu na kuwatesa,Sasa tunaona vitendo Vya uporaji  wa
Silaha katika vituo vyetu Vya polisi
Na wameenda Mbele zaidi kwa kuua watu kwa Risasi.

Tunaweza kuona baadhi ya matukio
Ya kusikitisha yaliyokwisha fanyika
Na WATU WASIO JULIKANA.

       (1) KUTEKWA NA KUTESWA KWA                  DR.ULIMBOKA
         
       (2) KUMWAGIWA TINDIKALI
               KWA SAID KUBENEA.

       (3)KUTEKWA NA KUNG'OLEWA
              JICHO KWA ABSLOM KIBANDA.

       (4)KUTOLEWA SILAHA                                     HADHARANI NAPE NNAUYE.

        (5)MAUAJI YA KIBITI

         (6) KUTEKWA NA KUUMIZWA
               ROMA MKATOLIKI

         (7) UPORAJI WA SILAHA KWENYE
               KITUO CHA POLISI
               SITAKISHARI

         (8)KUTEKWA KWA BEN SAANANE

          (9)KUUAWA KWA ALPHONCE
               MAWAZO.

          (10)UVAMIZI STUDIO ZA CLOUDS

           (11) KUPIGWA MABOMU OFISI
                   ZA IMMA ADVOCATE

            (12)KUPIGWA RISASI KWA
                   TUNDU LISSU.
 Hayo ni Matukio machache tu yanayo
Fanywa na WATU WASIO JULIKANA.

Ni muda Mwafaka sasa kila Mmoja
Kujitafakari hali hiyo mpaka lini?Watu
Wanao tenda hayo wapo kwenye jamii
Zetu,tuwafichue.
Tusipoungana kusaidiana na Vyombo
Vyetu Vya Ulinzi kesho inaweza
Kuwa zamu yako.Sababu inaonekana kabisa kuwa WATU HAO WASIO JULIKANA Dhamiri zao haziko hai
Tena.
        (1)Mtu asiye julikana.
  (2)Nape Nnauye akitolewa Silaha
      Na mtu asiye julikana
     (3) Alphonce Mawazo aliye uawa
           Mchana kweupe Na watu wasio                julikana.
       (4)Said Kubenea alimwagiwa                         tindikali na watu wasio julikana.
        (5)Absalom Kibanda aling'olewa
             Jicho na Watu wasio julikana.
         (6)Ben Saanane Ametekwa
              na Watu Wasio julikana,
               Mpaka leo haijulikani alipo.
       (7) Askari Polisi Wakiwa kibiti
            Kuwadhibiti Watu Wasio        
            Julikana.
        (8) Dr.Ulimboka alitekwa na
              Kuumizwa vibaya na
              Watu wasio julikana.
      (9) Roma Mkatoliki alitekwa
           Na kuumizwa vibaya na watu
            Wasio julikana.
(10)Tundu Lissu alipigwa
Risasi na Watu wasio julikana.

Thursday, 7 September 2017

BREAKING NEWS.

Tags
Mheshimiwa Tundu Lissu,Mbunge wa Singida Mashariki Amejeruhiwa kwa Risasi Mchana Huu mjini Dodoma.

Amekimbizwa katika Hospital ya Mkoa Wa Dodoma kwaajili ya Matibabu.

Monday, 4 September 2017

UCHAGUZI WA NAFASI YA URAIS NCHINI KENYA KURUDIWA MWEZI OCTOBER.

Tags
HABARI MPYA: Uchaguzi wa Urais Kenya utafanyika tarehe 17 mwezi Oktoba, wagombea wakiwa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta, Tume ya Uchaguzi IEBC yatangaza.

KWAYA YA BIKIRA MARIA MAMA WA MUNGU (BMM),PAROKIA YA YOMBO VITUKA WAREKODI NYIMBO ZA KUMUENZI MAMA BIKIRA MARIA.

Tags
   Kwaya ya Bikira Maria Mama wa Mungu iliyopo katika Parokia ya Yohana wa Mungu (Yohana de Deo)
Yombo Vituka Dsm,Wamerekodi Album mpya ya nyimbo za Bikira Maria

Akizungumza Mlezi wa Kwaya hiyo   Mr Kevin Mzelela,Amesema waliamua Kurekodi nyimbo hizo ambazo zote ni utunzi wa Nguli wa Muziki wa Dini Paschal Mwarabu ili Kutambua Mchango wa Mtunzi huyo katika Kanisa Katoliki.

  Mr.Kevin Mzelela ambaye amekuwa akiiwezesha Kwaya ya Bikira Maria Mama wa Mungu kufikia Malengo yake,amekuwa ni chachu ya Maendeleo ya Kwaya hiyo bila Kujibakiza,Ametoa wito Kwa watu wote wenye mapenzi mema  kuhakikisha wanapata nakala japo moja ya album hiyo itakayo zinduliwa hivi punde ili waweze kuonja radha Mpya ya Nyimbo hizo.


KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;

USIPANGE KUIKOSA