Padre Baptist Mapunda wa Kanisa Katoliki nchini, amtaka Rais John Magufuli kutambua kuwa bila majadiliano na viongozi wengine wa vyama vya siasa vya upinzani, hatma ya nchi itakuwa mbaya sana siku zijazo. Akitoa mahubiri yake katika Kanisa Katoliki la Manzese, jimbo kuu la Dar es Salaam jana, Padre Mapunda alisema Rais Magufuli awe na busara na kufuata mwenendo wa Nabii Suleimani ambaye katika uongozi wake alikuwa akiomba muongozo wa Mungu na hukujifanya Mungu mtu.
Kwa mujibu wa Padre Mapunda utekelezaji wa majukumu ya kiuongozi yanahitaji kusikilizana baina ya pande zinazokinzana pindi kunapokuwa na sintofahamu kama ilivyo sasa katika taifa.
“Hata Mungu aliwahi kukosolewa na Nabii Musa pale alipotaka kuwaondowa Waisraeli sembuse binadamu tunaoendelea kuishi au viongozi wetu? Hali hiyo inaonesha matakwa ya Katiba mpya yanahitajika kwa haraka sana”, Alisema Padre Mapunda.
Padre Mapunda aliwakumbusha viongozi wa dini wanaotarajia kukutana na rais Magufuli kumsaidia na kumuelekeza namna ya kuongoza nchi.
Alisisitiza kuwa Rais Magufuli na watendaji wake, wanapaswa kuiga mienendo ya Nabii Suleimani ambaye aliomba hekima na msaada kutoka kwa kwa Mungu katika kuongoza watu wake kwa HAKI na kutetea wanyonge.
"Watanzania wasome Biblia na kutambua mafundisho ya Yesu Kristo kwani alikuwa akifanya siasa ambazo zilitetea wanyonge lakini wanasiasa wetu wanapotosha umma, hivyo kanisa lazima likemee mwenendo ambao baadae utaichafua nchi ambayo ni kiota cha amani", Alisema Padre Mapunda.
Alisema, "Siasa bila dini ni sawa na wendawazimu na kusisitiza Nabii Suleimani anapaswa kuigwa na viongozi wa Tanzania kwa sababu katika utawala wake hakujifanya Mungu mtu".
Saturday, 9 September 2017
PADRE BAPTIST MAPUNDA (TUNDA LA KANISA)ATOA USHAURI MZITO KWA VIONGOZI WA SERIKALI.
Diterbitkan September 09, 2017
Tags
Artikel Terkait
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;
USIPANGE KUIKOSA
EmoticonEmoticon