HOTUBA YA MH MBOWE NA WANAHABARI
"Nianze na habari njema; Tundu Lissu anawasalimu sana. Nimeachana naye Nairobi jana mchana nikamwambia nitazungumza na Watanzania." Mbowe.
''TunduLissu hajawahi kukata kauli toka Siku ya kwanza ya shambulio na hata hali yake ya uelewa iko palepale'' Mbowe
''Mheshimiwa Lissu yupo chini ya ulinzi mkali sana, na hili limefanyika kutokana na watu waliokuwa wakitaka kumdhuru mh Lissu'' Mbowe
''Usalama wa Tundu Lissu ni mkubwa sana ndani na nje ya hospitali ya Nairobi masaa 24'' Mbowe
"Kumekuwa na kauli nyingi sana, ndugu zangu Watanzania pamoja na kiu ya kupata habari hili sio jambo la kuuzia magazeti'' Mbowe.
"Mashine yetu 'Lissu' itarudi barabarani salama kabisa ikiwa timamu, nataka niwaeleze ufahamu wake uko vizuri 100%" Mbowe
"Niwaombe rasmi kwa niaba ya Chama, madaktari, familia kuwaomba sana Watanzania, kauli zisizo rasmi zisipewe nafasi." Mbowe.
"Nisistize kwamba taarifa rasmi za chama zitatolewa na mimi mwenyewe nikiwa ama Dar es Salaam au Nairobi." Mbowe.
"Madaktari wanasema ni miujiza kutoka salama bila kukatwakatwa kwa risasi ktk shambulio kama la Lissu" Mbowe
"Lissu anatibiwa na kundi kubwa la madaktari na ningependa niwatambue waingie kwenye rekodi kwa kazi ya ziada kuokoa maisha ya Lissu." Mbowe
"Kazi kubwa iliyofanywa na madaktari wa dodoma tusiipuuze, ilituwezesha kufika Nairobi akiwa hai. Ilikuwa ni miujiza kila mmoja alishangaa." Mbowe
MBOWE;-kwenye kikao tulichokaa dodoma mimi pamoja na waziri wa afya Ummy Mwalimu,waziri wa mambo ya ndani,katibu wa bunge,naibu spika na spika wa bunge.
MBOWE.-Serikali iliweka msimamo kuwa kama lissu atapelekwa nairobi badala ya muhimbili haitakuwa tayari kugharamia matibabu ya lissu.
MBOWE;-Spika alitamka wazi kuwa bunge haliko tayari kugharamia matibabu ya lissu kama atapelekwa nairobi na spika alisema anajitoa na ananawa mikono.
MBOWE;-huyu ummy mwalimu aliyesema jana kuwa serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya lissu ndiye aliyeweka msimamo kuwa kama lissu atapelekwa nairobi basi serikali haiko tayari kugharamia matibabu yake.
MBOWE;-ummy mwalimu anasema wanaochangisha pesa za matibabu ya lissu ni matapeli mwambieni sisi hatuko kama wao waliokula pesa za rambirambi za kagera tutawatolea hesabu ya pesa zote za michango.
MBOWE-;mpaka sasa pesa ambazo wabunge walitoa nusu ya posho zao spika wa bunge amezitia mfukoni pamoja na kwamba aliomba acaunt ya hospital aziingize lakini mpaka leo spika hajaingiza hizo pesa ambazo wabunge walitoa kwa ajili ya matibabu ya lissu.
MBOWE;-Jaji mkuu suala ya uchunguzi si la mahakama ni la polisi wewe usubiri mahakamani tunakuheshimu sana ,tunapoomba uchunguzi kutoka nje ya nchi inamaana hatuna imani na vyombo vya ndani ..Kwa hiyo si vema sana jaji kutuingilia kwa hili..tunakuheshimu sana nisingependa kumvunjia heshima jaji huyu.
MBOWE-;spika alinipigia simu juzi kuwa wapo tayari kuhudumia kwa masharti matatu..Sharti la kwanza ni mbowe uandike barua ya maombi,,Sharti ya pili ni lissu lazima apelekwa india,,-Sharti la 3 familia iandike barua ya maombi.
MBOWE -;mbunge kutibiwa stahiki yake..mbunge hapaswi kuandika barua ya maombi kutibiwa kwake labda kama anaumwa mke wake au mtoto.
MBOWE-;mpaka sasa gharama za lissu kutibiwa ni zaidi ya milion 122,michango ya lissu ni dolla elfu 22 kutoka kwa watanzania wanaokaa nje,watanzania wa ndani wamechangia milion 54 za acaunt ya CRDB kwa njia simu ni milion 24.
MBOWE;-kuhusu ulinzi wa lissu msiwe na shida lissu analindwa 24 hours.
MBOWE-;Sisi kama binadamu tuna hisia kutokana na unyama tunaofanyiwa na serikali iliyopo madarakani ,Tuna hisi kuwa waliomshambulia lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama.
Friday, 22 September 2017
MBOWE AONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HALI YA MHE.TUNDU LISSU.
Diterbitkan September 22, 2017
Tags
Artikel Terkait
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;
USIPANGE KUIKOSA
EmoticonEmoticon