Charles Saasita Umeondoka bila
Kutuaga kaka? Mbona imekuwa
Ghafla kaka?
Wana Dar es saalam wanalia kaka,
Wana Arusha Hawaelewi nini kimetokea.
Mbona Juzi pale Arusha
Ulionekana mwenye Furaha tu kaka?
Wana C.M.O Tunalia,Wana Muziki Mtakatifu wanalia,wana Chang'ombe
Wanalia,wanachuo wa DUCE wanalia,Wapenzi wa nyimbo zako wanalia,Waumini wanalia,Nini kimekupata kaka?
Saasita,Hakika Umetuacha tumeduwaa,Naandika Machozi yananitoka Sababu Sijui nini kimekupata kaka?
Hatukusikia hata Neno lako la kutuaga kaka,Saasita Kanisa halielewi nini kimekupata,Kila Mmoja anashangaa.
Mwl Kacholi hajui nini kimetokea,Richard Mloka hajui nini kimekupata,Lucas Mlingi anashangaa Sababu jumapili ulikuwa naye lakini Leo anaandaa Mwili wako kwa safari huku ukiwa huwezi tena kusema Neno.David Wasonga Anauliza bila kupata majibu mlipoongea Majuzi kwenye simu ndo hamtaongea tena kupanga mipango ya kuboresha utunzi wa nyimbo?
Saasita Ni kweli hatutaona tena tungo zako Mpya? Waumini,wanakwaya,Rafiki zako,Majirani,Ndugu,Wazazi Nk.
Wote hawana Furaha tena.
Kaka Saasita, Nashindwa cha kuandika manake yaliyo tokea yanaleta Simanzi.
Kwa heri Saasita, Kwa heri ya kuonana.Siamini kama sitakuona tena.
UMETUTANGULIA MBELE NASI TUPO
NYUMA TUNAKUFUATA.
Msalimie Mzee Mgandu,Msalimie Mzee Syote,Msalimie Mzee Mkomagu,Msalimie Fr Kayeta
Wasalimie Wanamuziki Mtakatifu Woteee!
BURIANI CHARLES SAASITA.
Wednesday, 11 October 2017
CHARLES SAASITA NGULI WA MUZIKI MTAKATIFU, ALIYEZIMIKA KAMA MSHUMAA.
Diterbitkan October 11, 2017
Tags
Artikel Terkait
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;
USIPANGE KUIKOSA
EmoticonEmoticon