Mwanzoni Mwa Miaka ya 1950 kulikuwa na njaa kubwa,kiasi kwamba Wakazi wa Wilaya Ya Mbinga umatengoni Walilazimika kwenda Kufuata Mihogo Maeneo ya Ziwa Nyasa ili kunusuru maisha ya Familia zao.
Katika Familia ya Baba yangu pia walipata tatizo la Njaa lililo mfanya bibi yetu Afunge Safari ya Kwenda kufuata mihogo ziwa Nyasa.
Akiwa njiani katikati ya Msitu Mnene ghafla Watu wanne Walitokea Porini Wakiwa na Visu,Watu wale enzi hizo walijulikana kama "Chinja chinja".
Watu wale waliamua kutumia visu vyao kwa lengo la kutaka kumchinja bibi yangu.
Wakiwa katika haraka zao zile ghafla alitokea chui msituni,na kuanza kuwashambulia wale watu waovu.
Katika Purukushani zile Wale watu waovu wakakimbilia porini.Yule chui alipoona kuwa wale watu wamekimbia,
Akarudi tena barabarani na kuanza kumsindikiza bibi yangu mpaka karibu na makazi ya watu lakini bibi bado alikuwa na hofu juu ya chui na wale watu.Lakini baadaye aligundua kuwa kumbe yule chui alikuwa na Lengo la Kumwokoa dhidi ya Binadamu wenzake waovu,yule chui alipoona bibi yupo katika maeneo salama akatikisa mkia wake ishara ya kumuaga bibi naye akapotelea porini.Bibi alishangaa sana kitendo kile.
Naandika haya leo yaliyo tokea miaka ya 1950,nikitafakari mambo mengi.
(1)Karne hii watu wengine wanapowaza kukuza Uchumi na Teknolojia ktk nchi zao sisi tunawaza kuuana?
(2)Miaka ya 1950 Mnyama alimwokoa
Binadamu dhidi ya binadamu mwenzake sisi leo tunawaza kuuana?
(3)Karne hii Binadamu anaona bora kukutana na mnyama kuliko
Binadamu mwenzake?
(4)Karne hii Watu wanapolilia Amani sisi Tunataka kupoteza Amani?
(5)Karne hii Tunapoteza muda mwingi
Kuwaza namna ya kuwadhuru binadamu mwenzetu badala ya kuwaza juu ya maendeleo?
HAKIKA YATUPASA . KUBADILIKA,VINGINEVYO TUTAJUTIA HAYA YANAYO ZIDI KUKOMAA KILA UCHAO.
WATANZANIA HATUKULELEWA KATIKA HAYA YANAYO ENDELEA SASA, NI JUKUMU LA KILA MMOJA WETU KUPINGA HAYA KWA NGUVU ZOTE,BILA KUFANYA HIVYO TUTAJUTA.
Wednesday, 18 October 2017
TUNDU LISSU LEO UMENIFANYA NIYAKUMBUKE YALIYO MTOKEA BIBI YANGU ENZI HIZO.
Diterbitkan October 18, 2017
Tags
Artikel Terkait
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;
USIPANGE KUIKOSA
EmoticonEmoticon