Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo,Mheshimiwa Harrison Mwakyembe,Ijumaa ya Leo ametembelea Studio ya Highland
Iliyopo Maeneo ya Kigogo Dar es salaam,na Kufanya Maongezi na Mkurugenzi wake Engineer Richard Mloka.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa pongezi nyingi sana kwa Mkurugenzi wa Studio Hiyo Eng.Mloka,kwani Studio yake Imefanya kazi kubwa sana ya kukuza vipaji Vya wanamuziki Mbali mbali ktk Taifa Letu.
Studio Hiyo yenye Historia kubwa Katika Nchi ya Tanzania imekuwa kimbilio la Wanamuziki wa Nyimbo za kizazi kipya,Band Mbali Mbali ikiwemo TOT Band,lakini zaidi kabisa Studio hiyo ni Maarufu sana kwa Kurekodi Nyimbo za Kwaya Mbali Mbali Za kanisani.
Pamoja Na Kumiliki Studio Ya kurekodi Nyimbo,Engineer Richard Mloka anamiliki Pia Shule ya Muziki na Sound Engineering, Ambapo ni Chimbuko La Mafundi Mitambo Wengi Ambao baadhi Wanafanya Kazi Kwenye Vituo Mbali Mbali vya TV,kama Vile ITV na TBC na Wengine Kwenye Vituo Binafsi Na Studio Mbali Mbali.
(1) Waziri Mwakyembe akiwa na Mwenyeji Wake Eng.R.Mloka.
(2) Waziri Mwakyembe Akisistiza jambo.
EmoticonEmoticon