Wednesday, 30 August 2017

RADIO MAISHA FM YAJIDHATITI KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WATU WOTE.

Tags
Radio Maisha FM inayosikika kupitia 100.1MHz,Imejipanga kutoa Elimu ya Afya ili Kuokoa Maisha ya Watanzania.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Radio hiyo,Dr.Willifredius Rutahoile alipokuwa anaitangaza Radio hiyo kupitia MGUU KWA MGUU Promotion.

  Dr.Rutahoile Amesema kuwa aliamua
Kuanzisha Radio hiyo baada ya kuona kuwa Watanzania Wengi wanapoteza
Maisha kwasababu hawana Elimu ya kujikinga na Magonjwa Mbali Mbali yanayo wazunguka Katika jamii zao.

  Wananchi waliomshudia  Dr.Rutahoile  akiwa na baadhi ya Wafanyakazi Wa  Kituo hicho cha Radio,Wakiwa wamebeba Bango kubwa la kuitangaza Radio hiyo,Wametoa Pongezi nyingi sana kwa hatua hiyo ya Kuitangaza Radio hiyo kupitia MGUU KWA MGUU Promotion, kwani itakuwa Rahisi kwao kuuliza Maswali ya Papo kwa Papo ili kupata Elimu zaidi juu ya Afya Zao .

Radio hiyo inayosikika Katika Mji wa Dodoma na Baadhi ya mikoa ya Iringa Manyara,Morogoro na Singida,Tarehe 19/09/2017 itatimiza Mwaka Mmoja tangu Kuanzishwa Kwake.
             Dr.Rutahoile akiwa katika
             Moja ya Majukumu yake.
           Dr.Rutahoile akiwa katika
           Promotion ya MGUU KWA MGUU
     Baadhi ya Wafanyakazi wa Maisha          Radio Wakiwa katika MGUU KWA            MGUU Promotion.
        Wananchi Wakipata Maelezo toka
         Kwa Wafanyakazi wa MAISHA                  RADIO FM
 Hawa nao walifikiwa na MGUU KWA MGUU Promotion.

Thursday, 24 August 2017

AJALI MBAYA YAUA WANAFUNZI MOROGORO.

Tags
Kumetokea ajali Mbaya Asubuhi ya Leo Huko Morogoro,Ambapo Daladala ya kwenda Kihonda imegongana na Treini  na Kusababisha Vifo Vya Wanafunzi Ambao Idadi yao bado haija fahamika.



Tuesday, 22 August 2017

ABATE MTEULE PAMBO MARTIN OSB WA ABASIA YA MVIMWA KUSIMIKWA RASMI JUMAMOSI.

Tags
Shangwe,Ndelemo na Vifijo Vimetawala katika Mapokezi ya Abate Mteule Fr.Pambo Martin OSB wa Abasia ya Roho Mtakatifu Mvimwa-Sumbawanga.Idadi kubwa ya Watu walijitokeza kumpokea Abate Pambo Martin OSB akitokea Makao Makuu ya Shirika la Wabenedictine wa Mtakatifu Ottilia Huko Saint Ottilien Ujerumani,alikokuwa anafanya kazi kama Katibu Mkuu wa Shirika Hilo.
   Abate Pambo OSB ni Abate wa Tatu katika Abasia hiyo, Na atasimikwa Rasmi siku ya
Jumamosi Tarehe 26/08/2017 Huko Abasiani Mvimwa-Sumbawanga.
         (1) Abate Mteule  Akiwa kwenye                    Gari ya Wazi.
       (2)Gari ya Polisi ikiongoza                          Msafara wa Kumpokea                              Abate Mteule Pambo OSB.
        (3)Baba Askofu Damian Kyaruzi wa             Jimbo Katoliki la Sumbawanga                 Akiwa na Abate Mteule.

Monday, 21 August 2017

JE! WAJUA?

Tags
FAHAMU;Leo unaweza kuwasiliana na mtu yeyote duniani kutokana na ubunifu wa Alexander Graham Bell, ndiye aliyebuni simu ya umbali. (History.com)

Sunday, 20 August 2017

MHASHAMU BABA ASKOFU NGALALEKUMTWA AWAASA WAZAZI KUSAIDIA KUWALEA VIJANA WANAO JIUNGA NA MIITO MITAKATIFU.

Tags
     Augustine Kinunda; Iringa.

   Mhashamu Baba Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (T.E.C),Ametoa Wito kwa Waumini wa Jimbo la Iringa,Kuwapeleka Watoto wao Kujiunga na Miito Mitakatifu.Pia amesisitiza kuwa,hata Baada ya vijana Hao Kujiunga na Miito Mitakatifu, wasiache Waendelee kulelewa na Baba Askofu pekee,au na Walezi pekee,Kwani Suala la Malezi ni Jukumu la Wote.Baba Askofu Ngalalekumtwa pia Ametoa Wito kwa Waumini Wote Kuliombea Kanisa na Nchi yetu Dhidi ya Hila za Adui Shetani.Hayo yote Ameyasema Leo Katika Makazi yake yaliyopo Kihesa Iringa,Wakati akiongea na Wanakwaya wa Kwaya Ya Mtakatifu Sesilia Kihesa Iringa,walipoenda Asubuhi ya Leo Kumpa Pole,Baada ya Kupata Matatizo ya Afya,pia Msiba wa Pd.Ponsiano Myinga Aliye fariki kwa Ajali Wiki iliyopita.



Friday, 18 August 2017

DAR:MPAMBANAJI WA BIASHARA ZA PEMBE ZA NDOVU AUAWA KWA RISASI.

Tags
Mwanaharakati wa Kupambana na Biashara ya Pembe za Ndovu Wayne Lotter 51 auawa Kwa Risasi,Alikuwa Akishirikiana na Polisi Kukamata Wawindaji Haramu wa Tembo.Wayne Lo
tter 51 Aliuawa Akitokea Uwanja wa Ndege Kuelekea Nyumbani Kwake,Ambapo Gari aliyokuwa amepanda Ilizuiwa na Gari nyingine na ndipo Watu Wawili Wenye Bunduki Wakampiga Kwa Risasi na Hatimaye Kupelekea Kifo Chake.

MAJERUHI WA AJALI YA LUCKY VICENT WAREJEA.

Tags
Leo Imekuwa ni Siku Ya Furaha Kubwa kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Lucky Vicent Ya Arusha,na Watanzania Wote kwa ujumla;Baada ya Wanafunzi Walio Jeruhiwa katika Ajali Kurejea Nchini Mapema Leo Asubuhi. Katika kuonyesha Furaha yao Wanafunzi wa Shule hiyo Wameungana na Idadi Kubwa ya Wakazi Wa Arusha na viunga vyake,Kuwapokea Wanafunzi Hao Ambao Wamerejea Nchini Kwa Ndege Maalumu



toka Nchini Marekani Walikoenda Kwaajili Ya Matibabu.Tunashukuru Wamerejea Wakiwa na Afya Njema.

Wednesday, 16 August 2017

UKIKUTANA NA ENGINEER GEREON MMOLE UTAPENDA.

Tags
Ni Nadra Sana Nyakati Hizi Kukutana na Wataalamu Wa Muziki Ambao Pia Wanafanya Kazi zingine za kitaalamu.Engineer Wa Umeme Bwana Gereon Mmole ni Kati ya Wanamuziki Wachache ambao wana ujuzi Mwingine tofauti na Muziki.Binafsi nimevutiwa sana na Engineer Huyu Mchapa kazi,na Mnyenyekevu Hata kwa Wanafunzi Wake.Daima Awapo kazini Hakubali hata Dakika moja ipite bila kufanya jambo la Pekee la Kimaendeleo.Kiu yake kwa wanafunzi wake ni kuona kila Mmoja Anaelewa
 Kile Anacho Fundisha.Kwaujumla anaipenda kazi Yake lakini Pamoja na Kuipenda anaijua Vizuri sana Kazi yake,jambo linalo wafanya Hata Wanafunzi wake Wamwelewe kwa Urahisi.Engineer Mmole Anafundisha Chuo cha VETA Iringa,Lakini Pia ni Mtunzi Mahiri na Mkongwe Wa Nyimbo.

Tuesday, 15 August 2017

BREAKING NEWS.MOTO UMETANDA KATIKA SOKO LA SIDO MBEYA

Tags
Habari zilizo tufikia hivi Punde ni kwamba Moto Mkubwa Umetanda Katika Soko la Sido Mbeya,Na Vyombo Vya Ulinzi Vinazidi Kuimarisha Ulinzi wakati Jitihada za Kuzima Moto Huo zikiendelea.

MKUU WA MKOA DODOMA ATOA AGIZO ZITO.

Tags
Katika Kilele Cha Jubilei ya Miaka Miamoja ya Mapadre Tanzania, iliyofanyika Dodoma,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameagiza Ndani ya Siku Kumi na nne wahusika wa Kugawa Ardhi Wawe Wametoa Eneo Kwaajili ya Ujenzi wa Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Ambayo Yatahamishwa toka eneo la Kurasini Dar es salaam Kwenda Dodoma. Katika Maadhimisho hayo Mheshimiwa Waziri Simbachawene aliye Mwakilisha Mheshimiwa Rais John Pombe

Magufuli Amelipongeza kanisa Katoliki Kwa Kuhubiri Amani.Lakini Pia ametumia nafasi Hiyo kuwaongoza Waumini wa Kanisa hilo Kuwaomba Msamaha  Mapadre Kwa Makosa Yote waliyowatendea.Katika Kuunga Mkono Maaskofu Kwa Uamuzi wao wa Kuhamia Dodoma, Mheshimiwa Simbachawene, Amesema Badala ya Siku Kumi na Nne Yeye Amesema Ndani  ya Siku Kumi Maaskofu Wawe Wameulizwa ni Sehemu Gani Wao Wanatamani kujenga Hayo Makao Makuu Yao Katika Mji Wa Dodoma.

Saturday, 12 August 2017

WALES KARIA RAIS MPYA T.F.F

Tags
Bwana Wales Karia pichani Amechaguliwa Leo kuwa Rais Mpya Wa T.F.F,Katika Uchaguzi Uliofanyika Leo Katika Ukumbi Wa Saint Gasper Mjini Dodoma.Katika Uchaguzi Huo
Bwana Michael Wambura Amechaguliwa Kuwa Makamu Wake.

AJABU NA KWELI,MBWA MCHEZA PIANO NA KUIMBA.

Tags
Mbwa akicheza Piano na Kuimba.Hapo sasa wenzangu na Mimi Mnao Shindwa Kumwimbia Mungu Wakati Wa Ujana wenu.

ROMA AAMUA KUFUNGUKA YA MOYONI KUPITIA WIMBO NAKWENDA ZIMBABWE.

Tags

Friday, 11 August 2017

ROMA MKATOLIKI AFUNGUKA

Tags

Thursday, 10 August 2017

R.I.P FR.PONSIANO MYINGA

Tags
Padre wa Kanisa Katoliki Pd Ponsiano Myinga aliyefariki kwa ajali ya Gari




Siku ya Jumanne,Azikwa Leo Huko Tosamaganga Iringa.

WAGONJWA WA MACHO FULSA HIYOOOO.

Tags

Wednesday, 9 August 2017

KUISHI NI KUJIFUNZA:

Tags
Katika Maisha Ya Binadamu Hapa Duniani Zinahitajika Jitihada Za Pekee,Na hasa Jitihada Binafsi za Kujifunza Mambo Mbali mbali,ili Kufanya Maisha ya Baadaye Kuwa Rahisi Zaidi.Katika Zama Hizi Zenye Changamoto Nyingi Zinazo tokana na Utandawazi,vijana Wengi Hawataki kufanya Kazi Halali Zitakazo Wapatia Kipato Halali.Wengi Wanapenda Kuishi Maisha Mazuri kwa njia za mkato,Kitu Kinacho Wapelekea Kuingia katika Matatizo Mbali mbali.Vijana Wanao Jielewa Wanajitahidi Kujifunza Mambo Mbali mbali sasa,Ili kutengeneza Maisha Bora Yajayo,Kama wengi wanavyopenda Kusema "Mchumia Juani Hulia Kivulini".Vijana wa VETA Iringa Wana jitahidi Kusoma  Kwa bidii ili Kutengeneza Maisha Bora ya Baadaye. Hongereni sana Vijana Kwa Kutambua Thamani Ya Elimu.Hakika Kuishi ni Kujifunza.




Tuesday, 8 August 2017

AJALI MBAYA YAPOTEZA MAISHA YA PADRE WA KANISA KATOLIKI.

Tags
Watu Wawili Wamefariki Dunia,akiwemo Padre Ponsiano Myinga Wa Kanisa Katoliki Jimbo La Iringa Aliyekuwa Anafundisha Seminari Kuu Peramiho Songea,na Mama Mmoja aliyekuwemo Katika Gari Hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Padre Huyo.Pia Mtawa Mmoja wa Kike Wa Jimbo hilo
amejeruhiwa Vibaya Katika ajali hiyo,na Kukimbizwa Katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete.Chanzo Cha Ajali Hiyo iliyo husisha  Basi La Kampuni ya Upendo na Gari Aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na Padre Huyo ni Mwendo Kasi wa Dreva wa Basi Kwani ni Kawaida ya Madreva wanao endesha Mabasi yanayo pita katika bara bara Hiyo Kundesha Bila Tahadhari.

Monday, 7 August 2017

NGUVU YA KURA YAWAFANYA WAKENYA WAKESHE;

Tags
Katika Kile Kinacho Onekana Ni Kutambua Haki Yao Ya Kikatiba,Wakenya Wamekesha Katika Vituo Mbali Mbali Vya Kupigia Kura.Mpaka Sasa kuna Hali ya Manyunyu Ktk Baadhi Ya Maeneo  Nchini Kenya,Lakini Watu Wameendelea Kubaki Katika Mistari Kwa Utulivu Mkubwa.Katika Mataifa Mengi ya Afrika Kipindi Kama Hiki Wale Wanao Hitaji Kupigiwa Kura Wanajenga Urafiki na Wapiga Kura na Kuwapa Ahadi Kede Kede,Lakini Baada ya Kuchaguliwa Wanabadilika Kabisa na Hata Wakati Mwingine Kuzikana Ahadi Walizo Ahidi Wakati wa Kampeni.Hongereni Wakenya Tunaamini Mtachagua Kiongozi Atakaye Furahia Hali Bora ya Maisha ya Watu Wake,na Siyo Mtawala Atakaye Furahia Kukalia Kiti cha Utawala.

Sunday, 6 August 2017

SIKU YA UPASHANAJI HABARI DUNIANI;

Tags
Katika Jumapili Ya Upashanaji Habari Dunia,Baba Mtakatifu Fransis Ametoa Ujumbe Maalum Kwa Watu Wote Usemao "Msiogope,Nipo Pamoja Nanyi,Muwe na Matumaini" Msingi wa Ujumbe Huu ni Kwa sababu Siku Hizi Katika Vyombo Vingi Vya Habari,Habari zinazo tangazwa Sehemu Kubwa ni Habari Mbaya tu;Habari za Kuhuzunisha,Habari za Kukatisha Tamaa.(Vita,Mauaji,Matetemeko Ya ardhi,Nk)Baba Mtakatifu anatuasa tujitahidi  kupeana Habari Njema zenye Kuleta Matumaini ktk Jamii Zetu.Pia anatuasa Kutafsiri Kwa nia Njema Habari Mbali mbali Tunazopokea Kutoka Katika Vyanzo Mbali Mbali.

Friday, 4 August 2017

KWELI KUNA USALAMA HAPO?

Tags
Hii ni hatari kwa maisha.

Thursday, 3 August 2017

Pata hapa magazeti ya Leo

Tags












KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;

USIPANGE KUIKOSA