Katika Kilele Cha Jubilei ya Miaka Miamoja ya Mapadre Tanzania, iliyofanyika Dodoma,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameagiza Ndani ya Siku Kumi na nne wahusika wa Kugawa Ardhi Wawe Wametoa Eneo Kwaajili ya Ujenzi wa Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Ambayo Yatahamishwa toka eneo la Kurasini Dar es salaam Kwenda Dodoma. Katika Maadhimisho hayo Mheshimiwa Waziri Simbachawene aliye Mwakilisha Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli Amelipongeza kanisa Katoliki Kwa Kuhubiri Amani.Lakini Pia ametumia nafasi Hiyo kuwaongoza Waumini wa Kanisa hilo Kuwaomba Msamaha Mapadre Kwa Makosa Yote waliyowatendea.Katika Kuunga Mkono Maaskofu Kwa Uamuzi wao wa Kuhamia Dodoma, Mheshimiwa Simbachawene, Amesema Badala ya Siku Kumi na Nne Yeye Amesema Ndani ya Siku Kumi Maaskofu Wawe Wameulizwa ni Sehemu Gani Wao Wanatamani kujenga Hayo Makao Makuu Yao Katika Mji Wa Dodoma.
EmoticonEmoticon