Friday, 29 December 2017

ASIYE SIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU.

Tags
Anaandika Mch. Francis Mbalase wa Kanisa la Pentekoste -
Mbeya
Chonde chonde CCM,mmekosea kujibu maneno ya Askofu kwa matusi na kejeli. Kama mnajua kuombewa, pia mjue na kutubu. Kutubu sio dhambi ni kupatana na aliyekupa uhai.
Tunaofahamu mambo ya rohoni CCM mmekurupuka kumjibu Baba Askofu, mngejitathimini kwanza.Wala ktk hilo la Askofu, kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kujibu. Maana kukaa kimya nayo ni hekima.
Majibu mliojibu yote hayana mashiko na hayakujibu hoja za Askofu Kakobe (aibu tu)
Wapo viongozi wa dini wengi tu waliikemea serikali, waliopuuza waliiingiza jamii ktk utumwa wa kutawaliwa na taifa lingine.
Wakitubu Mungu aliwasamehe na kuwainulia kiongozi aliyewaokoa. Inamaana walipoingia utumwani, viongozi wale wakaidi walipoteza haki ya kutawala au kuuwawa.
Maaskofu wetu kuwaeleza kuwa mtubu wanawapenda sana, nia yao ni njema ili msiangamie. Badala yake mnawatusi,.. kweli?Mnawahoji kama wahalifu badala ya kuwaomba ushauri. Kiimani mnajipalia makaa ya moto. TUBUNI TU.
Musa alimkemea Farao mfalme wa Misri (Kut 10: 1-29), Elia Mtishbi alimkemea Ahabu (1Fal 17:1-24; 18:1-46) , Shadrack na wenzie (Dan 3:3-30) , Yohana mbatizaji kwa Herodi (Mt 14:1-12),Yesu mwenyewe alikemea mfalme kwa kumwita mbweha nk. (LK 13:31,32); Yohana Mbatizaji alionya askari na watumishi wengine wa Umma (mfano wa TRA leo yaani watoza ushuru) - LK 3:7-14.
Kiongozi yoyote wa kiroho ni wakili wa Mungu (kwa niaba ya Mungu). Ukisoma Tito 3:1 neno la Mungu linasema:
......UWAKUMBUSHE WATU KUNYEKEA KWA WENYE UWEZO NA MAMLAKA,NA KUTII,NA KUWA TAYARI KWA KILA KAZI NJEMA, na
WARUMI 13:1. Muagizaji wa haya au msimamizi ni mchungaji. Hivyo mambo yasipoenda sawa ni wajibu ayakemee maana yeye ni mamlaka ya mbinguni.
Tuondoe chuki na ukabila na udini ile Taifa letu Mungu aliinue. Naomba sasa watu wa madhehebu yote liombee sana Kanisa na Taifa na acheni kuombea watawala wasio na toba
1 Samweli 16:1 BWANA AKAMWAMBIA SAMWELI,HATA LINI UTAMLILIA SAULI,IKIWA MIMI NIMEMKATAA ASIWAMILIKI ISRAEL? Watu wasiokuwa na toba ni kuwaacha, maana hawawezi kwenda na BWANA.
MAASKOFU WOTE WAMESIMAMIA UTAIFA.Fahamu muda wote walikaa kimya,wameona uharibufu kuwa unakuja, tiini.
Ccm wamemkejeli Kakobe eti aache dini aje kwenye siasa. Naomba mfahamu kuwa siasa na dini vinakwenda pamoja na mtu wa dini hakwepi siasa. Najua hilo mnalijua sana na ndio sababu mkamteua Mchungaji Getrude Rwakatale kuwa mbunge. Mkisema mtumishi hahusiki na siasa,mnajionyesha mlivyo na unafiki. Bado hata wapinzani yupo Mch Msigwa. Kwa Askofu Kakobe imekuwa nongwa? Tena ameongelea mhimili wa taifa.
Mwisho niwaombe viongozi wangu, MTUBU TU.

Wednesday, 27 December 2017

Tags
http://sw.radiovaticana.va/news/2017/12/27/askofu_isaac_a_massawe_ateuliwa_kuwa_askofu_mkuu_jimbo_kuu_la_arusha/1356489

Tuesday, 26 December 2017

ASKOFU KAKOBE AIJARIBU SERIKALI.

Tags
   Askofu Kakobe Amewataka Viongozi wa Serikali Kuongoza kwa kufuata katiba ya Nchi.

Askofu Kakobe Akiwa anatoa Mahubiri yake Wakati wa Ibada ya Noeli,Amesema Viongozi wa Serikali Wanaongoza Nchi kwa kuto fuata Matakwa ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kwa kuzuia Vyama Vya Siasa kufanya kazi zake wakati vyama hivyo Vipo kikatiba.

  Askofu Kakobe Amesema Kutokana na Uvunjaji huo wa katiba ya nchi Kunaweza kuleta Mafarakano Ktk Nchi Kwani Amani iliyopo ni Matunda ya Waasisi wa Taifa hili Kuheshimu Katiba  na Sheria zilizozopo.

Pamoja na Hilo Askofu huyo ameishauri Serikali kama inaona Mfumo wa Vyama vingi haufai Bora kupeleka mswada Bungeni ili Itungwe Sheria ya kufuta Mfumo wa Vyama vingi ambao kwa sasa Katiba inautambua,Kwani Kuvizuia vyama hivyo kufanya kazi yake ni Kutenda Dhambi kwani hata Mungu pia Anaheshimu Sheria.

 Askofu Kakobe pia Amewashauri Viongozi kukubali kukosolewa kwani hata Mungu anasemwa vibaya Lakini Hawaadhibu Wanao Msema vibaya.

Tuesday, 21 November 2017

BREAKING NEWS! JENGO LA CLOUDS LINAUNGUA MOTO MUDA HUU.

Tags
Habari zilizo tufikia hivi punde,ni kwamba Jengo la Clouds Media linawaka Moto Muda huu,Chanzo cha moto huo hakija julikana bado.Jitihada za kuzima moto huo bado zinaendelea.

Monday, 13 November 2017

MSANII ELIZABETH MICHAEL "LULU" AHUKUMIWA KWENDA JELA.

Tags
 Mahakama Kuu Dar imemhukumu muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu', kifungo cha miaka miwili jela baada ya kumtia hatiani kwa kuua bila kukusudia.
Lulu amepewa adhabu hiyo
Baada ya kutuhumiwa kumuua bila kukusudia Msanii Mwenzake Steven Kanumba.

Thursday, 9 November 2017

TWENDE NA DON BOSCO KIMANGA.

Tags
UZINDUZI,UZINDUZI,UZINDUZI!

Kwaya Ya Don Bosco Parokia ya Tabata
Kimanga Dsm,Wanatarajia kufanya
Uzinduzi wa DVD yao iliyopewa Jina la         MUNGU ANATENDA MAAJABU.
Uzinduzi huo Utafanyika Tarehe 19/11/2017 Katika Ukumbi wa COMFORT HALL Tabata Shule. Waumini Wote Mnakaribishwa Kwenda kuwaunga Mkono katika kazi yao hii,yenye Ujumbe Mzuri wa kuleta Afya Bora  katika safari ya kiimani.Usikose pia kumtaarifu na Mwenzako ili Kwa Pamoja                           TWENDE NA DON BOSCO KIMANGA.


Picha zote kwa Hisani ya
Don Bosco Media.

Wednesday, 8 November 2017

Tags
http://estamalibiche.blogspot.com/2017/11/blog-post_8.html

Monday, 23 October 2017

PUMZIKA KWA AMANI BABA ABATE LAMBERT OSB.DUNIA ITAKUKUMBUKA DAIMA DUMU!

Tags

Na Peramiho Publications

“Namna gani mbona hamwelewi vijana!...... ” ni Maneno ya mzaha au masihara toka kwa aliyekuwa Abate wa tatu wa Abasia ya Peramiho, Emeritus Lambert (Helfried) Dorr (OSB) akiwa darasani na wanafunzi wa utawa, mwaka 2006 (Peramiho).

Uwezo wake wa kupandikiza elimu kwa wanafunzi wengi aliowahi kuwafundisha katika maisha yake wakiwemo wanafunzi wa Likonde pamoja na Abasia ya Peramiho, utakumbukwa daima  bila kificho, kwani waswahili wanasema “Kizuri kinajiuza, kibaya kinajitembeza”.

Safari ya maisha ya Padre Lambert ilianza mwaka 1936 katika kijiji cha Gerolzahn kwenye jimbo la Freiburg huko nchini Ujermani.  Mwaka 1956 alifanikiwa kufunga nadhiri  za muda baada ya kuaminiwa utawani.

Alipata fursa ya kupadirishwa Juni 29, 1960 baada ya kufuzu mafunzo yake vizuri. Alikuja Afrika (Afrika Mashariki) katika viunga vya Peramiho (Tanzania) mwaka 1964.

Akiwa mkoani Ruvuma alianza na kazi ya kufundisha katika Seminari ya Likonde huko Mbinga, kisha Mwaka 1970 alirudishwa Peramiho na aliendelea na kazi yake ya kufundisha katika Seminari ya Peramiho, wanafunzi wa utawa na kazi yake mama ya kutangaza neno la Mungu.

Desemba  08, 1976 alichaguliwa kuwa Abate wa tatu wa Abasia ya Peramiho lakini Kabla ya hapo alikuwa Priori wa Abasia hiyo hiyo ya Peramiho.

Kijiti cha Uabate alikipokea toka kwa Abate Eberhart Spiess OSB, huku Abate wa kwanza wa Abasia ya Peramiho akiwa ni Gallus Steiger OSB.

Lambert alipewa nafasi ya kuwa Abate wa Abasi ya Peramiho isyokuwa na kikomo, lakini yeye baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 30, mnamo mwaka 2006 aliamua kustaafu na kupisha nguvu mpya kwenye kiti hicho.

Kabla ya yeye kurudi Ujerumani mwaka 2015, baada ya kustaafu alienda kupumzika katika Monasteri ya Tororo (Uganda) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kisha mwaka 2008 akarudi Peramiho.

Awali Abate Lambert alipanga kuwa akifa azikwe Tanzania katika makaburi ya Abasia ya Peramiho hata hivyo kutokana na kusumbuliwa na mguu wake wa kushoto kwa muda mrefu madaktari walimshauri kwenda kupata matibabu nchini kwake Ujerumani kwa kuwa Tanzania hakuna hospitali inayoweza kumtibu.

“wakati wowote kabla ya mwisho wa mwaka huu natarajia kurudi nyumbani kwangu Ujerumani kwa ajili ya matibabu ya mguu wangu wa kushoto hivyo kwa kuwa matibabu hayo ni endelevu siwezi kurudi tena Tanzania’’,alisema Abate Lambert mwaka 2015.

Januari 04, 2015 akaagwa rasmi na waumini wa Parokia ya Peramiho katika kipindi ambacho wengi wao bado walikuwa wakiuhitaji msaada wake.

Abate Lambert alikuwa mwalimu wa somo la Historia ya Kanisa katika Seminari ya (Likonde) Kigonsera tangu mwaka 1964 amewafundisha viongozi mbalimbali wa Kanisa na serikali wakiwemo Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Norbert Mtega.

Kabla ya roho yake kuhitimisha safari yake ya hapa duniani Oktoba 22, 2017; mapema mwaka huu, akiwa nchini Ujerumani alipelekwa kwenye nyumba ya Wagonjwa katika Monesteri ya Munsterschwarzach kwa ajili ya matibabu zaidi. Hakika kazi ya Mungu haina makosa, Pumzika kwa amani Abate Lambert!
Moja ya watu ambao wameshtushwa na kifo chake ni Mwanafunzi wake Mtawa Fredrick Mwabena OSB aliyekuwa mwanafunzi wake wa Utawa toka mwaka 2006 hadi 2009 na amefafanua yafuatayo:

“Abate  Lambert Dorr OSB, Apumzike kwa Amani.  Babu na Mwalimu Wangu, wenyewe tulizoea kumwita Walking Encyclopedia maana alikuwa msomi wa kweli kweli”.

“Kazi yake ya  kuiendeleza Abasia ya Peramiho itakumbukwa daima hasa kuanza kuwapokea watawa wazalendo/Africans, 1982 suala ambalo halikuwepo kabla yake na kipindi hicho kilikuwa kigumu sana kwa watawa wazungu na waafrika kukaa nyumba moja lakini yeye alifanikiwa kuukata mzizi huo wa fitina”.

“Lambert alipenda watu wasome, kuna kipindi kuna Mtawa mmoja aliomba kwenda kusoma lakini utawala ulimcheleweshea majibu yake, akaamua kujifungia ndani siku tatu. Taarifa zilipomfikia Abate Lambert siku ya pili yake akapewa ruhusa ya kwenda shule”.

“Lambert  alikuwa mtu wa Sala, alikuwa mtu wa masihara, aliwapenda watu wa aina zote bila kuwabagua, alikuwa muwazi, vile vile alikuwa mshauri wa mambo ya taaluma hapa Tanzania”.

“Aidha namkumbuka Lambert alikuwa na sauti nzito sana, hapo Kanisani kwetu zile maiki hazikuwa na msaada kwake alikuwa na uwezo wa kuongea kwa sauti kubwa mno.

Mwisho alikuwa mpenzi sana wa kuvuta Kiko” alisimulia kwa masikitiko makubwa, Bro. Frederick Mwabena OSB.

Vile vile Kat. George Milinga alifafanua kwamba kifo cha Abate Lambert kimeliachia Kanisa pengo kubwa mno kwa kuwa amelifanyia mambo mengi mazuri:

“Yeye ametunza yatima wengi sana, nyumba nyingi za kitawa Kenya, Tanzania na Uganda zilijengwa na kufunguliwa wakati wa uongozi wake”.

“Alitumia fedha nyingi katika ujenzi wa Makanisa mfano Kanisa la Mbinga Mharule na kuwasaidia Mapadre na Makatekista na wakristo wengine; aliupenda upadre wake, utawala wake na mtu wa kutoa mahubiri yenye ujumbe mzito
”.
“Yeye alikuwa msomi na mwandishi wa vitabu vingi vya historia, vile vile alikuwa mwalimu wa somo hilo. Alikuwa mwanzilishi wa watawa waafrika wa kiume ambao tunawaona. Kabla yake walikuwepo watawa Wabenediktine Wamisionari wazungu tu!”.

“Yeye hakupenda makuu, aliishi na waafrika vizuri bila majivuno na alikuwa baba wa wote” anasisitiza mzee Milinga”.

Abate Lambert Yeye ni Msomi wa hali ya juu, alisoma Seminari Kuu ya Saint – Etienne na Voicebook, vile vile alipokuwa kwenye maandalizi ya kuja Afrika yeye na Padre Bonifaz Dinkel walipata fursa ya kwenda kusomea (Historia ya Kanisa) nchini Canada.

Atazikwa tarehe 27, 2017 siku ya Ijumaa huko Ujermani, wakati nchini Tanzania Tarehe 26, siku ya Alhamisi, Kanisa la Abasia ya Peramiho litafanya Misa maalum ya kumwombea.
“Kwa Maana huyu alionekana anampendeza Mwenyezi Mungu, akachukuliwa”

SOLI DEO HONOR ET GLORIA-KATIKA YOTE MUNGU PEKE YAKE ATUKUZWE.

Wednesday, 18 October 2017

TUNDU LISSU LEO UMENIFANYA NIYAKUMBUKE YALIYO MTOKEA BIBI YANGU ENZI HIZO.

Tags
Mwanzoni Mwa Miaka ya 1950 kulikuwa na njaa kubwa,kiasi kwamba Wakazi wa Wilaya Ya Mbinga umatengoni Walilazimika kwenda Kufuata Mihogo Maeneo ya Ziwa Nyasa ili kunusuru maisha ya Familia zao.

Katika Familia ya Baba yangu pia walipata tatizo la Njaa lililo mfanya bibi yetu Afunge Safari ya Kwenda kufuata mihogo ziwa Nyasa.

Akiwa njiani katikati ya Msitu Mnene ghafla Watu wanne Walitokea Porini Wakiwa na Visu,Watu wale enzi hizo walijulikana kama "Chinja chinja".

Watu wale waliamua kutumia visu vyao kwa lengo la kutaka kumchinja bibi yangu.

Wakiwa katika haraka zao zile ghafla alitokea chui msituni,na kuanza kuwashambulia wale watu waovu.

Katika Purukushani zile Wale watu waovu wakakimbilia porini.Yule chui alipoona kuwa wale watu wamekimbia,
Akarudi tena barabarani na kuanza kumsindikiza bibi yangu mpaka karibu na makazi ya watu lakini bibi bado alikuwa na hofu juu ya chui na wale watu.Lakini baadaye aligundua kuwa kumbe yule chui alikuwa na Lengo la Kumwokoa dhidi ya Binadamu wenzake waovu,yule chui alipoona bibi yupo katika maeneo salama akatikisa mkia wake ishara ya kumuaga bibi naye akapotelea porini.Bibi alishangaa sana kitendo kile.

Naandika haya leo yaliyo tokea miaka ya 1950,nikitafakari mambo mengi.

(1)Karne hii watu wengine wanapowaza kukuza Uchumi na Teknolojia ktk nchi zao sisi tunawaza        kuuana?

(2)Miaka ya 1950 Mnyama alimwokoa
     Binadamu dhidi ya binadamu                  mwenzake sisi leo tunawaza                       kuuana?

(3)Karne hii Binadamu anaona bora            kukutana na mnyama kuliko
      Binadamu mwenzake?

(4)Karne hii Watu wanapolilia Amani          sisi Tunataka kupoteza Amani?

(5)Karne hii Tunapoteza muda mwingi
    Kuwaza namna ya kuwadhuru                 binadamu mwenzetu badala ya               kuwaza juu ya maendeleo?

       HAKIKA YATUPASA                  .                   KUBADILIKA,VINGINEVYO                         TUTAJUTIA HAYA YANAYO ZIDI                 KUKOMAA KILA UCHAO.
        WATANZANIA HATUKULELEWA                KATIKA HAYA YANAYO ENDELEA           SASA, NI JUKUMU LA KILA MMOJA            WETU KUPINGA HAYA KWA                     NGUVU ZOTE,BILA KUFANYA                    HIVYO TUTAJUTA.



Wednesday, 11 October 2017

CHARLES SAASITA NGULI WA MUZIKI MTAKATIFU, ALIYEZIMIKA KAMA MSHUMAA.

Tags
Charles Saasita Umeondoka bila
Kutuaga kaka? Mbona imekuwa
Ghafla kaka?
Wana Dar es saalam wanalia kaka,
Wana Arusha Hawaelewi nini kimetokea.

Mbona Juzi pale Arusha
Ulionekana mwenye Furaha tu kaka?

Wana C.M.O Tunalia,Wana Muziki Mtakatifu wanalia,wana Chang'ombe
Wanalia,wanachuo wa DUCE wanalia,Wapenzi wa nyimbo zako wanalia,Waumini wanalia,Nini kimekupata kaka?

Saasita,Hakika Umetuacha tumeduwaa,Naandika Machozi yananitoka Sababu Sijui nini kimekupata kaka?
Hatukusikia hata Neno lako la kutuaga kaka,Saasita Kanisa  halielewi nini kimekupata,Kila Mmoja anashangaa.

Mwl Kacholi hajui nini kimetokea,Richard Mloka hajui nini kimekupata,Lucas Mlingi anashangaa Sababu jumapili ulikuwa naye lakini Leo anaandaa Mwili wako kwa safari huku ukiwa huwezi tena kusema Neno.David Wasonga Anauliza bila kupata majibu mlipoongea Majuzi kwenye simu ndo hamtaongea tena kupanga mipango ya kuboresha utunzi wa nyimbo?

Saasita Ni kweli hatutaona tena tungo zako Mpya? Waumini,wanakwaya,Rafiki zako,Majirani,Ndugu,Wazazi Nk.
Wote hawana Furaha tena.

Kaka Saasita, Nashindwa cha kuandika manake yaliyo tokea yanaleta Simanzi.
Kwa heri Saasita, Kwa heri ya kuonana.Siamini kama sitakuona tena.
  UMETUTANGULIA MBELE NASI TUPO
        NYUMA TUNAKUFUATA.
         Msalimie Mzee Mgandu,Msalimie             Mzee Syote,Msalimie Mzee                          Mkomagu,Msalimie Fr Kayeta
            Wasalimie Wanamuziki                             Mtakatifu Woteee!
           
             BURIANI CHARLES SAASITA.



Monday, 9 October 2017

Tags
*News Alert ! WATU ZAIDI YA NANE WAFARIKI BAADA YA HIACE KUTUMBUKIA ZIWA VICTORIA*👇👉 http://www.malunde.com/2017/10/news-alert-watu-zaidi-ya-nane-wafariki.html

Tuesday, 3 October 2017

VETA NYANDA ZA JUU KUSINI WAFANYA MAAJABU KATIKA MAONYESHO YA UTALII.

Tags
  VETA katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,Wamekuwa Washindi wa Pili katika Maonyesho ya Utalii yaliyo funguliwa na Waziri Prof.Jumanne Maghembe Tarehe 27/09/2017 na kufungwa na Waziri Augustine Maige
TAREHE 02/10/2017.

  Akiongea Mkuu wa Banda la VETA Mhandisi Gereon Mmole,alisema siri
Ya ushindi huo ni Kutokana na Umoja
Na mshikamano uliopo kati ya Walimu,
Wanafunzi, na Watumishi Wote wa VETA.

  Banda la VETA ambalo Muda Mwingi lilikuwa limesheheni Idadi kubwa ya
Watazamaji,lilikuwa ni kivutio kikubwa katika Maonyesho hayo,kutokana na Vifaa mbali mbali
Vya kuvutia Vilivyo tengenezwa na VETA.

Vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na Taa za kuongozea magari pamoja na Watumiaji wa bara bara,Swichi inayo washa taa baada ya Giza Kuingia na kujizima yenyewe baada ya Kutokea mwanga;Sahani zilizo tengenezwa kwa
Kuunganishwa vipande Vya mbao,kifaa maalum cha kuchomelea vyuma vyepesi,Bomba za kumwagilia bustani,Kifaa cha kupashia joto maji kwa kutumia mionzi ya jua,Pia Gari ya kufundishia Wanafunzi vilionekana kuwa kivutio kikubwa kwa Watu mbali mbali walio tembelea banda la VETA.

Kitu kingine ambacho ilikuwa ni kivutio kikubwa, ni kuona Wanafunzi wa VETA hasa wanafunzi wa kike ambao walikuwa mahiri katika kuelezea Namna Vifaa mbali mbali walivyo tengeneza vinavyoweza
Kufanya kazi.Wanafunzi hawa walikuwa chachu kwa baadhi ya Wazazi kukata shauri na kuamua kuchukua fomu ili watoto wao wakajiunge na VETA.Lakini Wanafunzi wa mambo ya mapishi walifanya watu wafurike katika banda la VETA kwenda kula chakula kitamu walichopika Wanafunzi hao Wakishirikiana na walimu wao.

Maonyesho haya  yamebadili mtazamo wa baadhi ya watu kuwa hakuna jambo lolote la Pekee linaloweza kufanywa na VETA. Wengi  wameshauri
Iwapo tunataka kweli kufikia uchumi wa viwanda,ni muda mwafaka sasa Serikali waiangalie VETA kwa jicho la pekee,kwani Kupitia VETA tunaweza kufanya mambo makubwa sana.
  (1) Cheti cha ushindi wa pili kwa VETA
  (2)Wanafunzi wa VETA wakiandaa               chapati.
     (3)Mmoja wa walio tembelea banda              la VETA akipata maelezo toka                      kwa Eng.Gereon Mmole.
   (4) Wanafunzi wa Udaktari toka                   UDOM wakiangalia Bomba za
        Kumwagilia bustani.
    (5) Wapo Makini kusikiliza maelezo            namna taa za kuwaongoza             .          watumiaji wa bara bara zinavyo
          Fanya kazi.
   (6) Walimu wa VETA na Wanafunzi
         Wakifurahia ushindi.
   (7) Maelekezo mbali mbali                              yakiendelea.
    (8)Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini          Mhe.Kasesela na Mgeni Rasmi                   Prof.Maghembe wakiangalia Gari ya
       Kufundishia.
   
    (9)Haamini kama VETA wanaweza              kutengeneza taa za kuongozea                  Magari
     (10) Mwanachuo yupo tayari kutoa
             Maelezo namna ya kutengeneza
             Batiki nzuri zisizo chuja.
    (11) Mwl Peter Kadala akiwa
            Tayari katika ofisi kwaajili ya                  kupokea Wageni
               Mbali mbali.
    (12) Idara ya kuzalisha Umeme kwa
            Mionzi ya jua (Solar Power)
            Wakitoa Maelezo ya namna
             Bora ya kuzalisha umeme huo.
    (13) Walimu wa Veta                                          wakibadilishana mawazo.
   (14) Akifurahia Maelezo Mazuri toka
        Kwa Mwanachuo.
  (15) Mwanachuo Fani ya Magari
          Akifafanua Mifumo ya magari.
   (16) Sahani zilizo tengenezwa kwa
          Vipande Vya mbao.
     (17)Mgeni Rasmi                                              Mhe.prof.Maghembe akiangalia
          Jiko lililo tengenezwa VETA.
   (18) Mkurugenzi Wa VETA kanda
          Akijadili jambo na Eng.Mmole
   19) Akiangalia Gari ya mafunzo.
    (20) Mashine ya kuchomelea vyuma
            vyepesi ikiwa katika majaribio.
   (21)Mkuu wa Chuo cha VETA Iringa  Eng.Raphael Ngwando Akifurahi baada ya kusikia Mgeni Rasmi akiimwagia sifa VETA kwa ubunifu.

Saturday, 30 September 2017

UTALII NI NGUZO YA UCHUMI WA VIWANDA.

Tags
Wapendwa Wananchi Wote Mnakaribishwa katika Maonyesho
Ya Utalii Yanayo endelea Katika
Viwanja Vya Kichangani vilivyopo
Kihesa Mkoani Iringa.

Kwa namna ya Pekee Tunawakaribisha
Katika Banda la VETA Mkoa wa Iringa,ili Mjionee Namna VETA inavyoweza Kuzalisha Mafundi wa Fani Mbali mbali.
   (1)Baadhi ya Bidhaa zilizotengenezwa         na Chuo cha VETA Iringa.
   (2) Mkuu wa Chuo Cha VETA                      Iringa,Eng Raphael Ngwandu                    akimtembeza Mgeni Rasmi                        Mheshimiwa Waziri Maghembe              alipotembelea banda la VETA.
      (3) Mwanachuo wa VETA                                 Iringa,Anatalia Luhala Akiwa                   na Batiki zilizo tengenezwa
             VETA.

  (4)Mkuu wa banda la VETA Mhandisi          G.Mmole akitoa                                             Maelekezo kwa mmoja wa walio             tembelea banda la VETA.
  (5)Wanachuo Fani ya Mapishi                        Wakiandaa Chakula kama sehemu
        Ya mazoezi kwao.

Thursday, 28 September 2017

MHASHAMU BABA ASKOFU SEVERIN NIWEMUGIZI ATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA ILIYOPENDEKEZWA NA TUME YA WARIOBA UENDELEE.

Tags


Askofu wa Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi.

Askofu Niwemugiza amesema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili, haki na ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.

Akifungua mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya leo Jumatano, Askofu Niwemugizi amesema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri.

Amesema hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye machafuko kwani wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.

Askofu Niwemugizi amesema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.



"Hizi sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni Katiba."

Amesema anatambua jitihada anazofanya Rais John Magufuli katika kupambana na ufisadi na kutaka rasilimali ziwanufaishe wanyonge lakini ni muhimu juhudi hizo zilindwe na Katiba nzuri.

"Rais anafanya mengi mazuri na alipoanza kila mmoja aliona dalili za matumaini lakini juhudi hizo zinaweza zisiwe endelevu kama hakuna ulinzi wa Katiba,”

"Tunahitaji Katiba tena Katiba nzuri ambayo haitaruhusu kuchezewa na yeyote kwa maslahi au matakwa yake binafsi."

Amesema, "Namshauri Rais achunguze kwa makini yatakayozungumzwa kwenye mkutano huu,  ayaone kuwa yana nia njema na ayafanyie kazi.

Tuesday, 26 September 2017

JE!UNAFAHAMU KUHUSU HII?

Tags
Inasemekana vita iliyopiganwa kwa muda mfupi zaidi hapa Duniani,ni kati ya Zanzibar na England. Iliisha ndani ya dakika 38 tangu kuanza kwake,vikosi Vya Askari wa Zanzibar viliamua kukubali kushindwa.Vita hii ilipiganwa mwaka 1896.

KWAYA YA MTAKATIFU SESILIA KIHESA WAMEKULETEA KALI ZAIDI;

USIPANGE KUIKOSA